• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Bukoba Municipal Council
Bukoba Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Mipango miji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo Uwekezaji
    • Ufugaji Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayotekelezwa
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mfuko wa Afya
      • Kodi ya Majengo
      • Hati Rasmi
    • Mpango Mkakati
      • Ripoti Mbalimbali
        • Council Annual Report
          • Kituo cha Habari
            • Taarifa kwa Umma
            • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
            • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
        • Quarterly Financial Report
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu Mbalimbali
      • Leseni ya Biashara
      • Fomu ya uadilifu
      • Fomu ya OPRAS
    • Ripoti Mbalimbali
      • Council Annual Report
        • Kituo cha Habari
          • Taarifa kwa Umma
          • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
          • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
      • Quarterly Financial Report
    • Miongozo mbalimbali
      • Kanuni za Uchaguzi
      • Mwongozo wa Kuendesha Tovuti
      • Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi na Salama ya Vifaa na Mifumo ya TEHAMA Serikalini
    • Bukoba MC Profile
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)

Maendeleo ya Jamii, Vijana na Ustawi wa Jamii

MAENDELEO YA JAMII, VIJANA NA USTAWI WA JAMII

Idara ya Maendeleo ya Jamii, Vijana na Ustawi wa Jamii ni miongoni mwa Idara zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kwa mujibu wa maelekekezo ya Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).Kuna sehemu tatu za kisekta kama ilivyoainishwa hapa chini;

Maendeleo ya Jamii kwa ujumla

Ustawi wa Jamii na

Vijana

MAJUKUMU YA IDARA 

Jukumu kuu la idara ni kutekeleza Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Jamii kwa kuhakikisha jamii ya Manispaa ya Bukoba inakuwa na ustawi na maendeleo kuanzia mtu mmoja mmoja, familia na jamii kwa ujumla.

MAJUKUMU YA SEHEMU YA MAENDELEO YA JAMII

Madhumuni ya Sehemu hii ni kuleta mabadiliko katika Jamii kwa kushirikisha wananchi, Serikali na Mashirika yasiyo ya Kiserikali katika nyanja za kiuchumi, kijamii, na kiutamaduni.

Majukumu na kazi kwa kila kitengo

Utafiti na mipango

Kukusanya, kuchambua na kuhakiki taarifa mbalimbali za kijamii kutoka mitaa na Kata na kupendekeza kushauri miradi mbalimbali kwa ajili ya wananchi,

Kuratibu shughuli za sehemu ya Maendeleo ya Jamii na kuziandikia mipango ya utekelezaji,

Kubuni mbinu mbalimbali za kushirikisha wananchi katika mipango ya maendeleo,

Kufanya utafiti wa awali na utafiti wa kina juu ya miradi inayopendekezwa na wananchi na kutoa taarifa,

Kutoa huduma kwa wananchi kupitia jumuiya, vikundi au binafsi vya uzalishaji na usimamizi wa miradi ya kiuchumi na kijamii

Kuandaa mafunzo ya watumishi wa sehemu ya maendeleo ya Jamii,

Kuandaa mafunzo kwa viongozi wa wananchi na makundi mbalimbali katika Jamii

Utunzaji wa Takwimu muhimu zinazohusu watu na mazingira yao mfano; idadi ya watu huduma za kijamii na kiuchumi zilizopo.

Uratibu wa Mpango wa TIBA kwa Kadi

Jinsia na maendeleo ya watoto

Kuratibu shughuli zote za maendeleo ya wanawake na watoto,

Kuingiza suala la jinsia katika mipango yote ya maendeleo ya jamii,

Kutoa mafunzo kwa wanawake kupitia vikundi vya uzalishaji mali na utoaji huduma juu ya wajibu na nafasi ya wanawake katika jamii,

Kutafuta kusimamia na kuratibu mikopo na misaada inayolenga kuleta kuleta ukombozi kwa wanawake,

Kusimamia kutekeleza sera za maendeleo ya wanawake na watoto katika kupiga vita umasikini na kuondoa suala la ajira kwa watoto.

Usajili wa Mashirika yasiyo ya Serikali (NGOs)

Kuratibu shughuli za usajili wa NGOs kuanzia ngazi ya mtaa, kata, Manispaa hadi Taifa.

Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu uboreshaji udhibiti na ubora wa takwimu zinazohusu mashirika yasiyo ya Kiserikali,

Kusimamia kwa karibu utendaji kazi wa mashirika yasiyo ya Serikali kwa kuzingatia mipangokazi iliyoainishwa baada ya kupata usajili,

Kuhakiki na kuratibu shughuli za jumuiya za watumia maji ngazi ya mtaa kata hadi Manispaa.

Kudhibiti UKIMWI

Kuratibu na kusimamia shughuli za mwitikio dhidi ya VVU/UKIMWI katika Halmashauri,

Kushirikiana na wadau (asasi na watu wanaoishi na vvu) kutengeneza mpango wa Halmashauri wa mwitikio wa VVU na UKIMWI,

Kuelimisha jamii juu ya mbinu za kujikinga dhidi ya maambukizi mapya ya VVU kwa kutumia njia mbalimbali kama sanaa shirikishi, sinema, semina, warsha nk,

Kuratibu ukusanyaji na utunzaji wa takwimu za huduma za UKIMWI kupitia mfumo wa TOMSHA

Kuimarisha shughuli a kiuchumi na kuongeza kipato kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI,

Kutoa misaada kwa makundi, familia na watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi

Sekta isiyo Rasmi

Kuainisha maeneo kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo kwa kushirikiana na sekta zingine

Kuandaa, kuratibu, kuwatambua na kuwaorodhesha wafanyabiashara walioko kwenye sekta isiyorasmi

Kuhamasisha uundaji wa vikundi vya wajasiliamali wa sekta isiyo rasmi

Kuandaa na kuendesha mafunzo ya wajasiliamali kuhusu uwekezaji, kudhibiti UKIMWI, jinsia na sheria mbalimbali za Halmashauri

Kuwaunganisha wajasiliamali wa sekta isiyo rasmi na wadau wengine ili waweze kutumia fursa zilizopo.

Kazi na Majukumu ya Sehemu ya Ustawi wa Jamii

Sehemu ya Ustawi wa Jamii ina wajibu wa kusimamia utoaji wa huduma za Ustawi wa Jamii kwa wananchi mbalimbali wenye matatizo ya kijamii yanayohitaji ufumbuzi wa Kiustawi. Huduma hizo zinatolewa kwa wananchi wa jinsi zote wakiwemo wazee, watu wenye ulemavu, watoto, wajane na wagane bila ubaguzi wa rangi na kabila.

Majukumu na kazi kwa kila kitengo

Huduma za ustawi wa familia na watoto

Kuratibu na kusimamia huduma zote zinazolenga kuimarisha ndoa na familia kwa ustawi wa wanandoa na watoto mfano; kuratibu mashauri ya ndoa, mashauri ya matunzo ya watoto ndani na nje ya ndoa, kuasili,nk.

Kuratibu usajili na ukaguzi wa vituo vya kulelea watoto wadogo mchana kwa mujibu wa sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009

Kuratibu usajili na ukaguzi wa makao ya kulelea watoto walio katika mazingira hatarishi kwa mujibu wa sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009

Kuratibu huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi kwa mujibu wa mpangokazi wa kitaifa wa kuhudumia watoto walio katika mzingira hatarishi

Kuratibu na kusimamia ulinzi na usalama kwa watoto kuanzia ngazi ya mtaa, kata na Halmashauri kupitia timu za ulinzi na usalama wa mtoto kwa mujibu wa sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 na kanuni za ulinzi na usalama wa mtoto.

Marekebisho ya tabia na haki za watoto kisheria

Kuratibu na kusimamia mabadiliko ya tabia kwa watoto walio katika mkinzano na sheria

Kuratibu na kusimamia haki za watoto walio katika mkinzano na sheria mbalimbali za nchi

Kuratibu na kusimamia kesi/mashauri yote ya watoto waliokatika mkinzano na sheria mahakamani

Kuratibu na kusimamia kesi/mashauri ya watoto waliguswa na sheria mahakamani.

Huduma za ustawi hospitali na vituo vya afya

Kuratibu na kusimamia huduma zote za kiustawi Hospitalini na katika viyuo vya Afya,

Kuratibu na kusimamia Msamaha wa matibabu kwa wagonjwa wasio na uwezo wa kugharamia matibabu,

Kuratibu na kusimamia dirisha la wazee hospitali na viyuo vya afya.

Utengamao wa Wazee na Watu wenye Ulemavu

Kuratibu na kusimamia utengamao kwa wazee na watu wenye ulemavu

Kuratibu na kusimamia vikundi, SACOS kwa watu wenye ulemavu

Kuratibu ukusanyaji wa takwimu za wazee na watu wenye ulemavu katika Halmashauri

Kuratibu mikopo midogomidogo kwa watu wenye ulemavu na wzazee.

Sehemu ya Vijana

Sehemu ya vijana inajukumu la kutoa huduma kwa vijana katika Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba huduma hizo ni pamoja;

Kuunda vikundi vya ujasiriamali,

Utoaji wa elimu ya uzazi wa Afya,

Stadi za kazi,

Ujasiriamali,

Madhara ya utumiaji wa madawa ya kulevya na kundi la vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi kama vile wanawake wanaojiuza.

Uratibu wa mikopo nafuu kwa vijana.

Watumishi walioko kwenye Idara

  • Idara ina watumishi 13 wenye majukumu kama yalivyoainishwa hapa chini;
  • Chacha J.S Mwita – Mkuu wa Idara
  • Richard George Salu – Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi
  • Japhet Kanoni – Afisa Ustawi wa Jamii wa Manispaa ya Bkoba
  • Consolata Sabino Kyando – Afisa Vijana wa Manispaa ya Bukoba
  • Diana Jasson – Afisa Ustawi wa Jamii
  • Murshid Issa – Afisa Maendeleo ya Jamii (Mratibu wa TASAF)
  • Peter Muchunguzi – Afisa Ustawi wa Jamii Msaidizi
  • Advela Ntangeki – Afisa Maendeleo ya Jamii Msaidizi
  • Shamila A. Hussein – Afisa Maendeleo ya Jamii Msaidizi
  • Tunza A. Japhari – Afisa Maendeleo ya Jamii Msaidizi
  • Merina S. Gombo – Afisa Maendeleo ya Jamii Msaidizi
  • Ester Christopher Mbwatila – Afisa Maendeleo ya Jamii Msaidizi
  • Michael Josia Kataraiya – Afisa Maendeleo ya Jamii Msaidizi

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA KUOMBA MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA NA HALMASHAURI KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU March 22, 2025
  • TERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BUKOBA MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA February 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI ASISITIZA UTUNZWAJI WA VIFAA VYA UANDIKISHAJI.

    April 29, 2025
  • MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI WALETA FARAJA KWA KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA MANISPAA YA BUKOBA

    April 16, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA BUKOBA AONGOZA KIKAO KUHUSU UTOAJI WA DOZI YA PILI YA CHANJO YA POLIO

    April 15, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, AFYA NA ELIMU YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA BUKOBA

    April 14, 2025
  • Angalia zote

Video

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba akitoa maelezo juu ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miradi ya Mbalimbali
  • Nyaraka mbalimbali
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu Huria

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bukoba Municipal Coucil

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 284 Bukoba

    Telephone: +255 28 2220226

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@bukobamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2017 Manispaa ya Bukoba .Haki zote Zimehifadhiwa