• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Bukoba Municipal Council
Bukoba Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Mipango miji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo Uwekezaji
    • Ufugaji Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayotekelezwa
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mfuko wa Afya
      • Kodi ya Majengo
      • Hati Rasmi
    • Mpango Mkakati
      • Ripoti Mbalimbali
        • Council Annual Report
          • Kituo cha Habari
            • Taarifa kwa Umma
            • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
            • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
        • Quarterly Financial Report
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu Mbalimbali
      • Leseni ya Biashara
      • Fomu ya uadilifu
      • Fomu ya OPRAS
    • Ripoti Mbalimbali
      • Council Annual Report
        • Kituo cha Habari
          • Taarifa kwa Umma
          • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
          • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
      • Quarterly Financial Report
    • Miongozo mbalimbali
      • Kanuni za Uchaguzi
      • Mwongozo wa Kuendesha Tovuti
      • Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi na Salama ya Vifaa na Mifumo ya TEHAMA Serikalini
    • Bukoba MC Profile
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)

Mifugo na Uvuvi

Mifugo na Uvuvi

UTANGULIZI:

 Mifugo na Uvuvi inaundwa na Sehemu kuu mbili  ambazo ni:-

(i) Mifugo

(ii) Uvuvi.

MAJUKUMU YA IDARA YA MIFUGO NA UVUVI KATIKA MANISPAA YA BUKOBA

Jukumu la Idara hii ni kutekeleza shughuli mbalimbali zinazohusiana na maendeleo ya mifugo na uvuvi kwa kushirikiana na Serikali kuu na Wadau kutoka Sekta binafsi. Shughuli zinazofanywa na Idara ni pamoja na:-

1. Maendeleo ya Mifugo
Kusimamia utekelezaji wa shughuli za Maendeleo ya mifugo na ufugaji kupitia huduma za ugani ikiwa ni pamoja na kuhamasisha uundwaji wa vikundi vya wafugaji. Kusimamia na kuratibu huduma za kinga na tiba kwa mifugo zitolewazo na Halmashauri ya Manispaa, Serikali Kuu na sekta binafsi. Kusimamia ukaguzi wa nyama na mazao yatokanayo na Mifugo usimamizi wa usafi wa mazingira ya machinjio yetu katika Manispaa. Kusimamia utoaji wa vibali mbali mbali vya kusafirishia mifugo na Mazao ya Mifugo ndani ya nchi na kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri na serikali kuu yanayotokana na mifugo na mazao yake.

  • Kuwatembelea wafugaji/Vikundi vya wafugaji ili kutoa ushauri wa kitaalam juu ya elimu bora ya ufugaji.
    maeneo yao ya kazi.
  • Kufanya utambuzi wa magonjwa, ufuatiliaji na utoaji chanjo dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mifugo ikiwa ni pamoja na kutoa matibabu ya mifugo na kufanya uchunguzi wa ugonjwa na ukaguzi wa afya ya mifugo na mazao yake
  • Kufanya ukaguzi wa nyama katika machinjio ya Rwamishenyi na Buhembe
    kila siku kuhakikisha usalama na usafi wa nyama.
  • Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa  miradi ya maendeleo ngazi za kata na Halmashauri
    Kufanya utambuzi na usajili wa mifugo na uwekaji chapa katika mifugo ikiwa pamoja na kuhuisha takwimu za mifugo


2. Uvuvi
Kusimamia shughuli za uvuvi wa ziwani ikiwa ni pamoja na kutoa leseni za uvuvi, kusajiri vyombo vya uvuvi, Kuhamasisha ufugaji wa samaki  katika mabwawa kwa lengo la kuinua kipato na lishe, Kusimamia soko la dagaa linalofanyika mara mbili kwa kila wiki katika eneo la forodhani, kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri yanayotokana na uvuvi,

  • Kusimamia sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2009.
  • kutoa kusimamia viwanda vya samaki na kusimamia wavuvi kupitia vikundi vya BMUs kuhakikisha wanafanya uvuvi endelevu. Ikiwa pamoja na kutoa elimu kwa vikundi vya kusimamia na kuendeleza rasilimali za Ziwa Victoria (BMUS) ili kufahamu faida za uvuvi endelevu na athari za uvuvi haramu
  • Kufanya doria za mara kwa mara nchi kavu na ziwani (Ziwa Victoria) kwa lengo la kupambana na uvuvi haramu.
  • Kutoa elimu ya ufugaji wa samaki katika mabwawa na katika ziwa (Fish caging)
  •  Utoaji wa leseni za Uvuvi
    - Leseni za biashara (Ukusanyaji) ya mazao ya samaki/dagaa/mabondo/mapanki
    - Leseni za Uvuvi
    - Usajili wa mitumbwi mipya na mitumbwi ya zamani
  • Kutoa vibali vya usafirishaji wa mazao ya uvuvi ndani na nje ya Manispaa ya Bukoba.


HUDUMA ZITOLEWAZO NA IDARA KATIKA MANISPAA YA BUKOBA
1. Utoaji wa vibali vya kusafirisha mifugo ndani na nje  ya Wilaya ya Bukoba
-  Ng’ombe/mbuzi na kuku katika manispaa  ya Bukoba
   Mfugaji au mtu yeyote anayehitaji kibali cha kusafirisha mifugo yake ndani ya Wilaya au nje ya Wilaya ya Bukoba ni sharti atimize        masharti yafuatayo ili aweze kupata kibali hicho

  • Kwa uhakika awe ndiye mwenye mali (mifugo) husika (kwa wafugaji) na kwa  wafanya biashara ya Mifugo ni sharti awe na Leseni ya biashara ya Mifugo pamoja na uthibitisho aliponunua hiyo mifugo hiyo.
  • Awe na uthibitisho wa kuthibitisha kuwa yeye ndiye mmiliki halali wa mali husika kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa uliothibitishwa na Afisa Mtendaji wa Mtaa/Kata (Kwa wafugaji)
  • Kwa mifugo ya Asili Mfugaji atatakiwa kuwa na kibali cha kuruhusiwa kuingiza mifugo kutoka  Serikali ya kijiji kule mifugo hiyo inakopelekwa kuonyesha uwepo wa eneo na malisho ya kutosheleza ziada ya hiyo idadi ya mifugo.
  • Awe na kibali cha Mtaalamu wa Idara ya Mifugo kuthibitisha afya ya mifugo yake
  • Awe na kiasi cha Tshs 1000/= kwa kila ng’ombe anayesafirishwa popote ndani ya wilaya na Tshs.1500/= kwa kila ng’ombe anayesafirishwa nje ya Wilaya lakini ndani ya Mkoa  na Tshs. 2500/= kwa mifugo inayosafirishwa nje ya Mkoa lakini ndani ya nchi.

    2. Utoaji wa vibali vya kusafirisha mazao ya samaki
          -  Idadi ya Kilo/Ujazo wa mazao yanayotarajiwa kusafirishwa
          -  Awe na leseni ya kufanya biashara ya mazao ya samaki (valid Licence)


Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA KUOMBA MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA NA HALMASHAURI KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU March 22, 2025
  • TERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BUKOBA MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA February 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI ASISITIZA UTUNZWAJI WA VIFAA VYA UANDIKISHAJI.

    April 29, 2025
  • MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI WALETA FARAJA KWA KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA MANISPAA YA BUKOBA

    April 16, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA BUKOBA AONGOZA KIKAO KUHUSU UTOAJI WA DOZI YA PILI YA CHANJO YA POLIO

    April 15, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, AFYA NA ELIMU YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA BUKOBA

    April 14, 2025
  • Angalia zote

Video

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba akitoa maelezo juu ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miradi ya Mbalimbali
  • Nyaraka mbalimbali
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu Huria

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bukoba Municipal Coucil

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 284 Bukoba

    Telephone: +255 28 2220226

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@bukobamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2017 Manispaa ya Bukoba .Haki zote Zimehifadhiwa