• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Bukoba Municipal Council
Bukoba Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Mipango miji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo Uwekezaji
    • Ufugaji Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayotekelezwa
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mfuko wa Afya
      • Kodi ya Majengo
      • Hati Rasmi
    • Mpango Mkakati
      • Ripoti Mbalimbali
        • Council Annual Report
          • Kituo cha Habari
            • Taarifa kwa Umma
            • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
            • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
        • Quarterly Financial Report
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu Mbalimbali
      • Leseni ya Biashara
      • Fomu ya uadilifu
      • Fomu ya OPRAS
    • Ripoti Mbalimbali
      • Council Annual Report
        • Kituo cha Habari
          • Taarifa kwa Umma
          • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
          • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
      • Quarterly Financial Report
    • Miongozo mbalimbali
      • Kanuni za Uchaguzi
      • Mwongozo wa Kuendesha Tovuti
      • Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi na Salama ya Vifaa na Mifumo ya TEHAMA Serikalini
    • Bukoba MC Profile
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)

RAIS SAMIA AMJENGEA NYUMBA BI CATHERINE NA WAJUKUU ZAKE SITA

Posted on: August 23rd, 2025

Mwandishi wetu Kagera.

*Bi. Catherine Nathahiel na wajukuu zake sita walipoteza makazi baada ya Nyumba waliyokuwa wakiishi awali kukumbwa na mafuriko yaliyotokea Manispaa ya Bukoba mkoa Kagera Mei 10,2024.

*Bukoba. Serikali imemkabidhi nyumba Bibi na wajukuu zake sita aliyojengewa na Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kupoteza makazi kwa mafuriko mwaka 2024.

*Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ilikumbwa na mafuriko makubwa Mei 10,2024 yaliyosababishwa na mvua iliyonyesha kwa wingi siku tatu mfululizo kisha kupelekea mto Kanoni kufurika na maji kuleta madhara kwa baadhi ya makazi ya watu wanaopakana na mto huo katika kata za Nshambya na Bilele.

*Aliyekuwa mkazi wa mtaa Migera, Kata Nshambya, Bi Catherine Nathahiel na wajukuu zake sita ni miongoni mwa wananchi waliyopata madhara ya nyumba yao waliyokuwa wakiishi awali kuporomoka na kusombwa na maji ya mafuriko.

Mkuu wa Mkoa Kagera, Mhe. Fatma Mwassa leo Jumapili, Agosti 24,2025 amemkabidhi Bi Catherine Nathahiel na wajukuu zake Sita kiwanja na nyumba yenye vyumba viwili vya kulala aliyojengewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan baada ya kupoteza makazi kwa mafuriko.

Amesema kiwanja na nyumba vimepatikana kwa gharama za Serikali ikiwa ni ahadi ya Rais Samia ili kunusuru familia hiyo ambayo haikuwa na makazi kamili ya kuishi tangu mwaka 2024.

Mwassa, licha ya kutotaja gharama zilizotumika kununua kiwanja na ujenzi ameongeza kuwa nyumba hiyo imejengwa katika Kiwanja kilichopimwa na Halmashauri na kupewa hati namba 102 kwenye kitaru F kata ya Buhembe Manispaa ya Bukoba.

"Kipindi hicho Baada ya kukagua athari za Mafuriko sisi kama Serikali tulibaini hii familia yenye wajukuu sita ilipoteza kila kitu na hatua zetu za haraka tulitoa msaada wachakula na vifaa vya shule kwa wanafunzi"

"Taarifa zilipomfikia Rais, Samia alitupatia maagizo kuwa familia hii yenye watoto sita waliyopoteza wazazi wote itafutiwe makazi ya kudumu kwa gharama za Rais na wasipelekwe vituo va kulelea yatima hivyo tumetekeleza na leo ndo maana tunawakabidhi nyumba na kiwanja hiki chenye hati" amesema Mwassa.

Mkuu wa wilaya Bukoba, Mhe. Erasto Sima awali akisoma taarifa fupi ya kukabidhi kiwanja na nyumba hiyo kwa Bibi Catherine na wajukuu zake sita amesema mpaka sasa familia hiyo ilikuwa inaishi kwa mtumishi wa Serikali idara ya afya Adelina Wilson tangu walipopata madhira hayo.

"Adelina aliwasaidia sehemu ya kuishi tangu alipogundua hawana msaada nasisi kama Serikali asingekuwa yeye na vyombo vya habari tusingejua kama kuna familia inateseka na aliomba aendelee kuishi nao mpaka leo" amesema.

Aidha, Bibi Catherine amemshukuru Rais Samia na Serikali kwa kuwakumbuka na kuwafuta machozi kwa kuwajengea nyumba hiyo na kuahidi kuendelea kuwatunza wajukuu zake kwa kulinda pia afya zao.

Ameongeza kuwa wajukuu zake anaishi nao kwasababu amepoteza mme wake muda mrefu na vijana wake watatu tegemezi waliyofariki ambao walikuwa wazazi wa watoto.

Bibi Catherine, wajuu zake wanne ni wakiume na wawili wakike miongoni mwao mmoja wao ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya Sekondari Hamugembe, Loveness Matungwa amesema nikama muujiza maana tangu wamewapoteza wazazi wao hawakutegemea kama siku moja watalala sehemu salama kama nyumba waliyojengewa na Rais Samia.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA KUOMBA MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA NA HALMASHAURI KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU March 22, 2025
  • TERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BUKOBA MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA February 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • TAFUTENI FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA MAENEO YENU. MJUNGU

    August 28, 2025
  • RAIS SAMIA AMJENGEA NYUMBA BI CATHERINE NA WAJUKUU ZAKE SITA

    August 23, 2025
  • KAGERA KUJA NA MPANGO MKAKATI KUPUNGUZA UDUMAVU

    August 14, 2025
  • RC. KAGERA AWATAKA WAKANDARASI WA MIRADI YA TACTICS KUKAMILISHA KAZI KWA WAKATI NA UBORA

    July 23, 2025
  • Angalia zote

Video

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba akitoa maelezo juu ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miradi ya Mbalimbali
  • Nyaraka mbalimbali
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu Huria

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bukoba Municipal Coucil

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 284 Bukoba

    Telephone: +255 28 2220226

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@bukobamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2017 Manispaa ya Bukoba .Haki zote Zimehifadhiwa