• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Bukoba Municipal Council
Bukoba Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Mipango miji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo Uwekezaji
    • Ufugaji Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayotekelezwa
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mfuko wa Afya
      • Kodi ya Majengo
      • Hati Rasmi
    • Mpango Mkakati
      • Ripoti Mbalimbali
        • Council Annual Report
          • Kituo cha Habari
            • Taarifa kwa Umma
            • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
            • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
        • Quarterly Financial Report
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu Mbalimbali
      • Leseni ya Biashara
      • Fomu ya uadilifu
      • Fomu ya OPRAS
    • Ripoti Mbalimbali
      • Council Annual Report
        • Kituo cha Habari
          • Taarifa kwa Umma
          • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
          • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
      • Quarterly Financial Report
    • Miongozo mbalimbali
      • Kanuni za Uchaguzi
      • Mwongozo wa Kuendesha Tovuti
      • Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi na Salama ya Vifaa na Mifumo ya TEHAMA Serikalini
    • Bukoba MC Profile
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)

RC. MWASSA AFUNGUA MAFUNZO YA WAHESHIMIWA MADIWANI, AWASISITIZA ZAIDI UPENDO NA MSHIKAMANO.

Posted on: February 2nd, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Hajjat Fatma Mwassa amefungua rasmi mafunzo maalum kwa Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri za Manispaa ya Bukoba, Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba pamoja na Missenyi, akiwataka kuzingatia misingi ya upendo, mshikamano na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuwasimamia wananchi na miradi ya maendeleo.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, RC Mwassa alisema kuwa madiwani wana nafasi kubwa na ya kipekee katika kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi kwa wakati na kwa ufanisi, kwani wao ndio wawakilishi wa moja kwa moja wa wananchi katika ngazi za Serikali za mitaa.

Amesisitiza kuwa bila mshikamano na ushirikiano miongoni mwa Madiwani, viongozi wa Halmashauri na Wataalamu, utekelezaji wa miradi ya maendeleo unaweza kukumbwa na changamoto zisizo za lazima. “Upendo na mshikamano ni nguzo muhimu katika uongozi. Bila hivyo, hata rasilimali zilizopo haziwezi kuleta matokeo yaliyokusudiwa” amesema RC Mwassa.

RC Mwassa amewataka Madiwani kuwa sauti ya kweli ya wananchi waliowachagua kwa kusikiliza kero, maoni na mapendekezo yao, na kuyawasilisha kwa ujasiri katika vikao halali vya maamuzi. Aidha, amewakumbusha kuwa dhamana waliyopewa na wananchi inapaswa kulindwa kwa vitendo, uadilifu na uwazi.

Katika mafunzo hayo ambayo yatafanyika kwa siku tatu kwenye ukumbi wa Mikutano wa ELCT Bukoba Mjini, mada mbalimbali zinatarajiwa kujadiliwa ikiwemo usimamizi wa miradi ya maendeleo, matumizi sahihi ya rasilimali za umma, maadili ya uongozi, pamoja na majukumu na mipaka ya viongozi wa kuchaguliwa katika ngazi za Halmashauri.

Kwa upande wao, baadhi ya Waheshimiwa Madiwani walioshiriki mafunzo hayo wameeleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu katika kuwajengea uwezo na kuwapa mwelekeo wa pamoja katika utekelezaji wa majukumu yao, hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inaendelea kusisitiza uwajibikaji na thamani ya fedha.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa madiwani na kuchangia kwa kiasi kikubwa kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huku yakilenga kuimarisha mahusiano mema kati ya viongozi na wananchi wanaowawakilisha

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA KUOMBA MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA BA HALMASHAURI KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU December 12, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE SEMINA KWA AJILI YA UCHAGUZI MKUU OKTOBA, 2025. October 20, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI UCHAGUZI MKUU 2025 October 02, 2025
  • TANGAZO LA KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA KUOMBA MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA NA HALMASHAURI KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU September 15, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC. MWASSA AFUNGUA MAFUNZO YA WAHESHIMIWA MADIWANI, AWASISITIZA ZAIDI UPENDO NA MSHIKAMANO.

    February 02, 2026
  • WAZIRI NANAUKA AVUTIWA NA UBUNIFU WA VIJANA KONGANI YA BUKOBA MANISPAA

    January 25, 2026
  • KAMATI YA LISHE BUKOBA MANISPAA YAWEKA MIKAKATI YA KUHANIKIZA CHAKULA MASHULENI

    January 16, 2026
  • "TUILINDE AMANI TULIYONAYO" MBUNGE WA JIMBO LA BUKOBA MJINI

    November 28, 2025
  • Angalia zote

Video

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba akitoa maelezo juu ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miradi ya Mbalimbali
  • Nyaraka mbalimbali
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu Huria

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bukoba Municipal Coucil

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 284 Bukoba

    Telephone: +255 28 2220226

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@bukobamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2017 Manispaa ya Bukoba .Haki zote Zimehifadhiwa