• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Bukoba Municipal Council
Bukoba Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Mipango miji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo Uwekezaji
    • Ufugaji Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayotekelezwa
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mfuko wa Afya
      • Kodi ya Majengo
      • Hati Rasmi
    • Mpango Mkakati
      • Ripoti Mbalimbali
        • Council Annual Report
          • Kituo cha Habari
            • Taarifa kwa Umma
            • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
            • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
        • Quarterly Financial Report
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu Mbalimbali
      • Leseni ya Biashara
      • Fomu ya uadilifu
      • Fomu ya OPRAS
    • Ripoti Mbalimbali
      • Council Annual Report
        • Kituo cha Habari
          • Taarifa kwa Umma
          • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
          • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
      • Quarterly Financial Report
    • Miongozo mbalimbali
      • Kanuni za Uchaguzi
      • Mwongozo wa Kuendesha Tovuti
      • Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi na Salama ya Vifaa na Mifumo ya TEHAMA Serikalini
    • Bukoba MC Profile
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)

Walengwa wa TASAF Manispaa ya Bukoba wapokea mil. 112.8

Posted on: March 21st, 2018

Walengwa wa TASAF Manispaa ya Bukoba wapokea mil. 112.8

Manispaa ya Bukoba imeendelea kuneemesha walengwa wa mpango wa TASAF kwa kuwapatia shilingi  milioni 112,856,000. Uhawilishaji fedha huo wa ni dirisha la 17 tangu TASAF ianze rasmi na unafanyika kwenye mitaa 45 katika kata mbalimbali. Mradi umelenga kuwasaidia walengwa hao kuboresha makazi, kuanzisha ujasiriamali na/au kuboresha miradi yao ya kilimo na kadharika.

Akizungumza kwenye kikao cha maandalizi ya uhawilishaji fedha na wawezeshaji ngazi ya Wilaya kilichofanyika kwenye Ofisi ya TASAF Machi 14 mwaka huu, Mratibu wa TASAF wa Manispaa ya Bukoba Bw. Japhet Kanoni, amewataka wawezeshaji wakatoe semina kwa walengwa juu ya matumizi sahihi ya fedha  za mpango.

“Wajitahidi kuanzisha miradi midogo midogo kama ya ujasiriamali au waboreshe miradi yao ya kilimo lakini pia wafanye ukarabati maeneo yao ya kuishi na kuna wengine ambao wanaweza kuingia kwenye miradi ya ufugaji na kadharika”  alisema  Kanoni, na kuwaasa kuwa kuna shughuli inaendeshwa na maafisa ugani kwa kila mtaa ambao watawapitia walengwa hao, wahakikishe wanawaonyesha miradi yao ili wapatiwe ushauri wa kitaalamu utakaofanya miradi yao iwe na tija.

Kanoni anaendelea kusisitiza kwamba watoto wote ambao wameandikishwa shule na wanaohudhuria kiliniki, wasikose kwenda shuleni au kiliniki. Wakikosa kuhudhuria watasababisha fedha zao zipungue au zikatwe kwa sababu ya kutotimiza mashariti ya mpango huo.

Uelimishaji kwa walengwa umefanyika kwa siku nne kuanzia  machi 15hadi 19 mwaka huu ambazo zilikuwa siku za uhawilishaji fedha katika mitaa tofauti tofauti.

Miongoni mwa Walengwa walioshiriki mafunzo hayo na kupokea fedha ya mpango huo ni kutoka mitaa ya Kafuti, Buyekera, Nyakanyasi, Zamzam, Omukigusha, Bulibata, Kyasha, Ntungamo, Omukituli, Anyama,Uhuru , Forodhanu, Kabangamilembe, Nyangoye, Omukishenye, Ijuganyondo B, Kabalekangaiza, Kagondo kaifo, Kaluguru, Kyamuzinga na Bushwa. Mitaa mingine ni pamoja na Kyaya, Makongo, Rwazi, Katatolwanso, Kisindi, Matopeni, Rwome, Nyamulugo,Bugambakamoi,Busimbe A, Busimbe B, Kagemu, Kalelabana, Kyamuhumula, Msira, Nyamukazi, Bunkango, Bushaga, Ihyoro, Kyamyosi, Nyarubanja,Rubumba, Kamizilente na Rwamishenye.

Kwa upande wa walengwa wa mpango huo, wameishukuru na kuisifia Serikali ya awamu ya tano kwa kuwakumbuka katika dirisha la 17 huku wakiwahakikishia wawezeshaji ngazi ya Wilaya kuwa Serikali itegemee matokeo chanya hasa baada ya mafunzo hayo ya mara kwa mara ya  kuwajengea uwezo.

“Mimi napenda kuishukuru TASAF kwa kuwa tulikuwa tunaishi kwenye nyumba ya nyasi lakini sasa tushaezeka bati na tumenunua mbuzi mmoja” alisema Bi Modesta Koku Joseph kutoka mtaa wa Bulibata kata ya Buhembe. Halikadhalika amewashauri walengwa wengine wa mpango watumie fedha wanayopokea kulingana na malengo yaliyokusudiwa.

Mlengwa kutoka mtaa wa Nyakanyasi, Bi Winifrida Sylivesta Mutakangwa anashukuru Serikali. Yeye alikuwa hana mtaji lakini kuptia TASAF amepata mtaji na anafanya biashara ndogo ndogo ya kuuza samaki.

“Kwa upande wangu kwa kweli nimenufaika na mpango kwa sababu sikuwa na mtaji ambao ulikuwa umekamilika, niliongeza mtaji sasa nanunua samaki nabanika, nilinunua wavu na vifaa vingine vya kutumia   na mambo mengine ” alisema Winifrida Sylivesta Mutakangwa.

Fedha hizo zimetolewa kwa walengwa 3,190 kutoka mitaa 45. Hata hivyo, fedha iliyotolewa na Serikali shilingi 112,856,000 ni dirisha la 17 la uhawilishaji fedha, ikiwa na lengo la kuwafanya walengwa wajinasue kwenye dimbi la umasikini.


Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA KUOMBA MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA NA HALMASHAURI KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU March 22, 2025
  • TERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BUKOBA MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA February 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI ASISITIZA UTUNZWAJI WA VIFAA VYA UANDIKISHAJI.

    April 29, 2025
  • MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI WALETA FARAJA KWA KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA MANISPAA YA BUKOBA

    April 16, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA BUKOBA AONGOZA KIKAO KUHUSU UTOAJI WA DOZI YA PILI YA CHANJO YA POLIO

    April 15, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, AFYA NA ELIMU YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA BUKOBA

    April 14, 2025
  • Angalia zote

Video

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba akitoa maelezo juu ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miradi ya Mbalimbali
  • Nyaraka mbalimbali
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu Huria

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bukoba Municipal Coucil

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 284 Bukoba

    Telephone: +255 28 2220226

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@bukobamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2017 Manispaa ya Bukoba .Haki zote Zimehifadhiwa