• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Bukoba Municipal Council
Bukoba Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Mipango miji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo Uwekezaji
    • Ufugaji Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayotekelezwa
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mfuko wa Afya
      • Kodi ya Majengo
      • Hati Rasmi
    • Mpango Mkakati
      • Ripoti Mbalimbali
        • Council Annual Report
          • Kituo cha Habari
            • Taarifa kwa Umma
            • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
            • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
        • Quarterly Financial Report
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu Mbalimbali
      • Leseni ya Biashara
      • Fomu ya uadilifu
      • Fomu ya OPRAS
    • Ripoti Mbalimbali
      • Council Annual Report
        • Kituo cha Habari
          • Taarifa kwa Umma
          • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
          • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
      • Quarterly Financial Report
    • Miongozo mbalimbali
      • Kanuni za Uchaguzi
      • Mwongozo wa Kuendesha Tovuti
      • Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi na Salama ya Vifaa na Mifumo ya TEHAMA Serikalini
    • Bukoba MC Profile
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)

DC. SIMA AKEMEA TABIA YA WANAWAKE KUTELEKEZA WATOTO WACHANGA.

Posted on: March 8th, 2025

Mkuu wa WIlaya ya Bukoba Mhe. Erasto Sima amewakemea wanawake wote wenye tabia ya kuwatelekeza watoto wachanga punde tu wanapojifungua na kupotelea kusikojulikana.

Sima ameyasema hayo wakati akitoa hotuba yake kwenye sherehe za maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambayo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba imefanyika kwenye viwanja vya Mayunga.

Ameeleza kuwa, tabia hii ya wanawake kutelekeza watoto wachanga imeendelea kushika hatamu ambapo imepelekea watoto wengi kukosa malezi ya Mama na hivyo kupelekwa kwenye vituo vya kulelea watoto yatima.

“Pamoja na umuhimu wa siku hii kubwa kimataifa, bado Wanawake mmekuwa na dosari kadhaa ambazo lazima tuziseme. Tabia ya wanawake wachache kuwatupa watoto wachanga imeendelea kumea hapa Bukoba na mimi nikiwa kama Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama, Wilaya tunajipanga vyema ili kuwatafuta wale wote wanaofanya kitendo hiki kibaya. Alisema Mkuu wa Wilaya.

Akisisitiza kuhusu ukatili huu DC. Sima alisema, “Ndugu zangu Wanawake, hili jambo sio jema, Wiki iliyopita kwenye moja ya Kata zetu, kimeokotwa kichanga kidogo kimeshafariki kitu ambacho hakileti picha nzuri, zaidi sana hata mwezi uliopita, kiliokotwa kichanga ambacho kilitelekezwa kwenye banda la kuuzia nyanya na mpaka sasa bado kinaendelea vizuri pale hosipitali ya Zamzam, Kwa hiyo ndugu zangu niwaombe muache tabia hii mara moja”

Nayo Idara ya Maendeleo ya Jamii, Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba wakiwa katika maandalizi ya siku hii muhimu kwa Wanawake, iliweza kuwaunganisha wanawake mbalimbali na kutembelea kituo cha kulea watoto yatima cha Ntoma kilichopo Maruku tarehe 6/3/2025 na kutoa misaada mbalimbali kabla ya kuandaa kongamano la Wanawake mashsusi kwa ajili ya kuzungumzia fursa mbalimbali ambazo wanawake wanatakiwa kuzichangamkia lakini pia kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili.

Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake yamefanyika Jijini Arusha na mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Datari Samia Suluhu Hassan na yakiongozwa na kauli mbiu isemayo, “Wanawake na Wasichana 2025, Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA KUOMBA MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA NA HALMASHAURI KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU March 22, 2025
  • TERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BUKOBA MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA February 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI ASISITIZA UTUNZWAJI WA VIFAA VYA UANDIKISHAJI.

    April 29, 2025
  • MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI WALETA FARAJA KWA KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA MANISPAA YA BUKOBA

    April 16, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA BUKOBA AONGOZA KIKAO KUHUSU UTOAJI WA DOZI YA PILI YA CHANJO YA POLIO

    April 15, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, AFYA NA ELIMU YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA BUKOBA

    April 14, 2025
  • Angalia zote

Video

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba akitoa maelezo juu ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miradi ya Mbalimbali
  • Nyaraka mbalimbali
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu Huria

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bukoba Municipal Coucil

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 284 Bukoba

    Telephone: +255 28 2220226

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@bukobamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2017 Manispaa ya Bukoba .Haki zote Zimehifadhiwa