• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Bukoba Municipal Council
Bukoba Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Mipango miji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo Uwekezaji
    • Ufugaji Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayotekelezwa
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mfuko wa Afya
      • Kodi ya Majengo
      • Hati Rasmi
    • Mpango Mkakati
      • Ripoti Mbalimbali
        • Council Annual Report
          • Kituo cha Habari
            • Taarifa kwa Umma
            • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
            • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
        • Quarterly Financial Report
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu Mbalimbali
      • Leseni ya Biashara
      • Fomu ya uadilifu
      • Fomu ya OPRAS
    • Ripoti Mbalimbali
      • Council Annual Report
        • Kituo cha Habari
          • Taarifa kwa Umma
          • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
          • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
      • Quarterly Financial Report
    • Miongozo mbalimbali
      • Kanuni za Uchaguzi
      • Mwongozo wa Kuendesha Tovuti
      • Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi na Salama ya Vifaa na Mifumo ya TEHAMA Serikalini
    • Bukoba MC Profile
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)

DC. SIMA AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA MKATABA WA LISHE NGAZI YA KATA MANISPAA YA BUKOBA

Posted on: May 10th, 2025

Bukoba, 10 Mei 2025* — Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mhe. Erasto Sima, ameongoza kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mkataba wa afua za lishe ngazi ya Kata kwa robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2024/2025 kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba.

Kikao hicho kimewakutanisha viongozi mbalimbali wakiwemo Katibu Tawala wa Wilaya, Bi. Proscovia Jaka Mwambi, wakuu wa idara na vitengo kutoka sekta ya elimu ya msingi na sekondari, mchumi wa Halmashauri pamoja na watendaji wa Kata.

Akitoa taarifa ya hali ya utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe, Afisa Lishe wa Manispaa ya Bukoba, Bi. Gisera Richard, amesema kikao hicho kimelenga kuchambua changamoto zilizopo na kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha matokeo ya utekelezaji wa afua za lishe katika ngazi ya jamii.

“Miongoni mwa malengo yetu ni kuhakikisha viashiria vyote vya lishe vinafikiwa kwa ufanisi na kwa ushirikiano wa sekta zote zinazohusika,” alieleza Bi. Afisa Lishe.

Katika taarifa yake, Bi. Gisera aliainisha baadhi ya mafanikio yaliyopatikana hadi kufikia robo hii ya mwaka, ikiwemo ongezeko la utoaji wa elimu ya lishe mashuleni na usambazaji wa virutubisho kwa watoto chini ya miaka mitano. Hata hivyo, alibainisha pia changamoto kadhaa kama vile uhaba wa rasilimali fedha, ufuatiliaji hafifu wa baadhi ya maeneo, na uelewa mdogo wa jamii kuhusu lishe bora.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya, Mhe. Sima, alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya viongozi wa kata na jamii katika kuhakikisha kuwa afua za lishe zinafikiwa kwa walengwa wote, hasa watoto, wajawazito, na akina mama wanaonyonyesha.

“Lishe bora ni msingi wa afya na maendeleo ya taifa. Tunapaswa kushirikiana kwa karibu kuhakikisha kila mtoto anapata haki yake ya lishe bora,” alisema Mhe. Sima.

Bi. Proscovia Jaka Mwambi alihimiza watendaji wa kata kuwa mabalozi wa mabadiliko katika maeneo yao kwa kuhakikisha taarifa sahihi za lishe zinafika kwa wananchi na kuchochea mabadiliko chanya ya tabia.

Kikao hiki ni mfululizo wa mikutano ya tathmini inayolenga kuimarisha utekelezaji wa mkataba wa lishe kwa ushirikiano wa sekta mbalimbali kama elimu, afya, na maendeleo ya jamii ili kuhakikisha kuwa Bukoba inasonga mbele katika mapambano dhidi ya utapiamlo.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA KUOMBA MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA NA HALMASHAURI KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU March 22, 2025
  • TERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BUKOBA MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA February 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • DC. SIMA AONGOZA KIKAO CHA TATHMINI YA MKATABA WA LISHE NGAZI YA KATA MANISPAA YA BUKOBA

    May 10, 2025
  • AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI ASISITIZA UTUNZWAJI WA VIFAA VYA UANDIKISHAJI.

    April 29, 2025
  • MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI WALETA FARAJA KWA KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA MANISPAA YA BUKOBA

    April 16, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA BUKOBA AONGOZA KIKAO KUHUSU UTOAJI WA DOZI YA PILI YA CHANJO YA POLIO

    April 15, 2025
  • Angalia zote

Video

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba akitoa maelezo juu ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miradi ya Mbalimbali
  • Nyaraka mbalimbali
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu Huria

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bukoba Municipal Coucil

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 284 Bukoba

    Telephone: +255 28 2220226

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@bukobamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2017 Manispaa ya Bukoba .Haki zote Zimehifadhiwa