• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Bukoba Municipal Council
Bukoba Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Mipango miji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo Uwekezaji
    • Ufugaji Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayotekelezwa
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mfuko wa Afya
      • Kodi ya Majengo
      • Hati Rasmi
    • Mpango Mkakati
      • Ripoti Mbalimbali
        • Council Annual Report
          • Kituo cha Habari
            • Taarifa kwa Umma
            • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
            • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
        • Quarterly Financial Report
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu Mbalimbali
      • Leseni ya Biashara
      • Fomu ya uadilifu
      • Fomu ya OPRAS
    • Ripoti Mbalimbali
      • Council Annual Report
        • Kituo cha Habari
          • Taarifa kwa Umma
          • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
          • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
      • Quarterly Financial Report
    • Miongozo mbalimbali
      • Kanuni za Uchaguzi
      • Mwongozo wa Kuendesha Tovuti
      • Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi na Salama ya Vifaa na Mifumo ya TEHAMA Serikalini
    • Bukoba MC Profile
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)

DKT. BITEKO APONGEZA TAMASHA LA IJUKA OMUKA

Posted on: December 19th, 2024

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajjat Fatma Mwassa kwa maandalizi mazuri ya Kongamano la Uwekezaji mkoani humo litakaloibua fursa za uwekezaji na kukuza uchumi wa mkoa.

Dkt. Biteko ametoa pongezi hizo leo Desemba 19, 2024 mkoani Kagera wakati akizungumza katika Tamasha la Pili la Uwekezaji la mkoa huo ikiwa sehemu ya Wiki ya Ijuka Omuka (Kumbuka Nyumbani).

“Nawapongeza waandaaji wa Kongamano hili na kama kuna watu wamekuja kuwekeza hapa napenda kuwapongeza wale mlioitikia wito tangu kwenye kongamano la kwanza na kuja kuwekeza hapa, Maombi yangu baada ya mkutano huu waje wengine kuwekeza na tutumie fursa hii ya uwepo wa mkoa huu kijiografia na kutumia fursa zilizopo,” amesema Dkt. Biteko.

Aidha, amewaasa wananchi wa Mkoa wa Kagera kuunga mkono jitihada za Mkuu wa Mkoa na kumpa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza majukumu yake.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Innocent Bashungwa amesema chimbuko la Tamasha hilo ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyetaka ifanyike tathmini ili kujua sababu za kudorora kwa uchumi na maendeleo ya Mkoa wa Kagera. Amesema mnamo mwaka 2022 wadau walikutana na kuainisha chanzo cha mkwamo kama mkoa.

“ Wananchi wa Kagera tuna bahati ya kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa Rais Samia na utashi wake wa kisiasa kuhusu mkoa wetu kutupa miradi mbalimbali ya maendeleo na hivyo inatupa fursa zaidi ya kukuza uchumi wetu,” amesema Mhe. Bashungwa.

Ameendelea kueleza kuwa sababu za kijigrafia kwa mkoa wa Kagera pia zinauweka katika nafasi ya kimkakati kuleta maendeleo "Kijiografia tunamshukuru Mungu mkoa wetu upo eneo la kimkakati na tuna rasilimali watu wa kutosha hivyo tunawakumbusha wenzetu waliopo maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi kukumbuka nyumbani licha ya majukumu yao huko walipo,”

Mhe. Bashungwa ameishukuru Serikali kwa utekelezaji wa miradi mikubwa kama vile ujenzi wa daraja la Kigongo - Busisi ambalo linatarajiwa kuzinduliwa mwezi Februari 2025, ujenzi wa barabara na pamoja na kuzungumizia hitaji la mkoa wa Kagera kuingia kwenye Gridi ya Taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Hajjat Fatma Mwassa amesema kuwa lengo la Tamasha hilo la Pili la Uwekezaji la Mkoa wa Kagera ni kutoa fursa kwa Serikali na mrejesho kwa wadau juu ya mafanikio na mipango ya Serikali kuhusu uchumi wa Mkoa huo.

Akielezea wasilisho lake la miradi na fursa zilizopo mkoani humo, ametaja baadhi ya miradi inayoendelea kutekelezwa kuwa ni ujenzi wa barabara za kimkakati zenye urefu wa km 265.4 zinazogharimu shilingi bilioni 340.49 na ujenzi wa madaraja matano utakaogharimu shilingi bilioni 45.2.

Miradi mingine ni vituo vinne vya umeme vilivyojengwa kwa shilingi bilioni 163.

Katika sekta ya kilimo, Mhe. Mwassa amesema mkoa wake una mikataba miwili ya miradi ya umwagiliaji inayogharimu shilingi bilioni 2.9.

Halikadhalika, mkoa huo unatekeleza miradi mikubwa ya maji itakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 191 na kunufaisha zaidi ya wananchi 500,000.

Ameendelea kusema Mkoa huo umepakana na nchi jirani nne na mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria na hivyo kuwahakikishia soko la uhakika wa bidhaa.

Aidha, amewapongeza wawekezaji mkoani humo kwa kujenga viwanda baada ya kuvutiwa na fursa zilizopo mkoani humo.

Pia, ametoa wito kwa wananchi kufuga samaki na dagaa kwa vizimba na kuongeza thamani ili waweze kuuza nje ya nchi badala ya sasa ambapo wanunuzi toka nje huenda kununua dagaa moja kwa moja kwa wafugaji wadogo.

Mhe. Mwassa amehamasisha uwekezaji wa hoteli mkoani humo “Mikutano hii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki haifanyiki hapa Kagera kwa sababu hatuna uwezo wa kuhudumia idadi kubwa ya watu, mfano Polisi kutoka nchi hizi za Jumuiya ya Afrika Mashariki walipenda kuja hapa kufanyia mkutano wao haikuwezekana kwa sababu hatuna ukumbi wa kuhifadhi watu 3,000 kwa pamoja hivyo walienda mahali pengine” amebainisha Mhe. Mwassa.

Vilevile, Mhe. Mwassa ameonesha kiu yake ya kuona uwanja wa ndege wa Omukajunguti ukijengwa na kukamilika ili kutoa huduma kwa wananchi na kuchochea ukuaji wa uchumi wa mkoa huo.

Mhandisi kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Emannuel Mayanga amesema kuwa kupitia Miradi ya Kupendezesha Miji (TACTIC) kwa manispaa ya Bukoba ni ujenzi wa barabara zenye urefu km 10.75, uwekaji wa zaidi ya taa za barabarani zaidi 800 zitakazosaidia kuangaza Bukoba wakati wa usiku, uboreshaji wa kingo za Mto Kanoni pamoja na uboreshaji wa soko.

Kupitia tamasha hilo wadau na wawekezaji wamefanya majadiliano kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo mkoani humo.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA KUOMBA MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA NA HALMASHAURI KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU March 22, 2025
  • TERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BUKOBA MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA February 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI ASISITIZA UTUNZWAJI WA VIFAA VYA UANDIKISHAJI.

    April 29, 2025
  • MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI WALETA FARAJA KWA KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA MANISPAA YA BUKOBA

    April 16, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA BUKOBA AONGOZA KIKAO KUHUSU UTOAJI WA DOZI YA PILI YA CHANJO YA POLIO

    April 15, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, AFYA NA ELIMU YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA BUKOBA

    April 14, 2025
  • Angalia zote

Video

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba akitoa maelezo juu ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miradi ya Mbalimbali
  • Nyaraka mbalimbali
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu Huria

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bukoba Municipal Coucil

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 284 Bukoba

    Telephone: +255 28 2220226

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@bukobamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2017 Manispaa ya Bukoba .Haki zote Zimehifadhiwa