• Wasiliana nasi |
    • Maswali |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Bukoba Municipal Council
Bukoba Municipal Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara/Vitengo
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Mipango miji
      • Afya
      • Elimu ya Sekondari
      • Elimu ya Msingi
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Usafi na Mazingira
      • Kitengo cha TEHAMA
      • Uchaguzi
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Nyuki
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo Uwekezaji
    • Ufugaji Uwekezaji
  • Huduma
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Ratiba ya Vikao vya Wah. Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayotekelezwa
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
      • Mfuko wa Afya
      • Kodi ya Majengo
      • Hati Rasmi
    • Mpango Mkakati
      • Ripoti Mbalimbali
        • Council Annual Report
          • Kituo cha Habari
            • Taarifa kwa Umma
            • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
            • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
        • Quarterly Financial Report
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Fomu Mbalimbali
      • Leseni ya Biashara
      • Fomu ya uadilifu
      • Fomu ya OPRAS
    • Ripoti Mbalimbali
      • Council Annual Report
        • Kituo cha Habari
          • Taarifa kwa Umma
          • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
          • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)
      • Quarterly Financial Report
    • Miongozo mbalimbali
      • Kanuni za Uchaguzi
      • Mwongozo wa Kuendesha Tovuti
      • Mwongozo wa Matumizi Bora, Sahihi na Salama ya Vifaa na Mifumo ya TEHAMA Serikalini
    • Bukoba MC Profile
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Umma
    • Video za shughuli za Ofisi/Kitaifa
    • HOTUBA YA MHESHIMIWA KASSIM M. MAJALIWA (MB.)

RC. Mwasa aipongeza Manispaa ya Buko ba kwa kupata hati safi.

Posted on: May 26th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Hajat Fatuma Mwasa, ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba kwa kupata hati safi na hoja chache kuliko halmashauri zote.

Hajat Mwasa, amesema hayo katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano, tarehe 26 May 2024.

Amesema miaka mitatu ijayo Manispaa hiyo itakuwa imeimarika zaidi ikiongeza kasi ya kukusanya mapato ya ndani huku akiwaasa, Mkurugenzi na Watumishi wote waanze mikakati ya kuzuia hoja kwa sababu zikiibuka maana yake wamekiuka taratibu na miongozo iliyopo.

Katika kueleza hilo, Mkuu wa Mkoa alitolea mfano wa hoja iliyojitokeza ya miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.1 ambayo haijakamilika.

Hata hivyo amewataka pia kuzingatia thamani ya fedha na miradi inayoibuliwa ya maendeleo, ambapo ameeleza kuwa changamoto ni mapato ya ndani kuwa madogo kwa sababu mikoa mingine fedha za miradi kutoka serikali kuu ikichelewa huwa wanatumia mapato hayo.

Hivyo amewataka wahakikishe wanaongeza mapato ya ndani ili kuweza kumalizia miradi viporo ambayo ipo kwenye kata zetu, hapa Manispaa.

Amesema jukumu kubwa katika kukusanya mapato ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara ambapo hizo milioni 432 ambazo hazikukusanywa zingesaidia katika miradi ya maendeleo.

“Hatuwezi kufanya maendeleo bila kukusanya kodi hata wafanyakazi tunakatwa kodi asilimia 30 ya mishahara yetu, ”amesema Mkuu huyo wa Mkoa.

Awali akisoma taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2022/23 kwa niaba ya Mkurugenzi, Mwekahazina wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Bi. Flora Lengwana, amesema jumla ya hoja zilizoibuliwa ni 21 kati ya hizo 4 zimetoka miaka ya nyuma na hoja 17 ni mpya .

Lengwana, amesema hoja zilizojibiwa kikamilifu ni 12 na hoja 9 utekelezaji wake unaendelea huku zinazoendelea ni pamoja na mfumo wa ukusanyaji mapato kutokuwa sawa, mapungufu katika kuibua vyanzo vya mapato ya ndani, mapungufu katika mfumo wa tehama (watumishi wa tehama kutopata mafunzo).

Amesema hoja zingine zinazoendelea pia kutokukamilika kwa miradi ya maendeleo yenye thamani ya shilingi milioni 300 ambapo Mkaguzi amemshauri Mkurugenzi kuitengea bajeti ya kukamilisha miradi hiyo.

Amesema miradi ya miaka ya nyuma ambayo imetelekezwa bila kukamilika yenye thamani ya bilioni 2.22 ambayo haijakamilika waitafutie fedha na kuikamilisha ili isiendelee kuibua hoja kila mwaka.

Katibu Tawala Mkoa wa Kagera Stephen Ndaki, amewataka kuanzisha mkakati wa kuzuia hoja katika Manispaa hiyo na kuwa makini katika kila hatua za kutekeleza miradi ya maendeleo na kuibua vyanzo vipya vya mapato ya ndani bila kuibua hoja zisizokuwa za lazima.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo Jacob Nkwera ,amesema hoja zote zilizoibuliwa na Mkaguzi atazipatia ufumbuzi ambapo mwaka wa fedha ujao miradi viporo ya maendeleo imepewa kipaumbele.

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUFUNGULIWA KWA DIRISHA LA KUOMBA MIKOPO YA 10% INAYOTOLEWA NA HALMASHAURI KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU March 22, 2025
  • TERMS OF REFERENCE FOR THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN BUKOBA MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 10, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI February 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA February 05, 2025
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • AFISA MWANDIKISHAJI MSAIDIZI ASISITIZA UTUNZWAJI WA VIFAA VYA UANDIKISHAJI.

    April 29, 2025
  • MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI WALETA FARAJA KWA KAMATI YA FEDHA NA UTAWALA MANISPAA YA BUKOBA

    April 16, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA BUKOBA AONGOZA KIKAO KUHUSU UTOAJI WA DOZI YA PILI YA CHANJO YA POLIO

    April 15, 2025
  • KAMATI YA UCHUMI, AFYA NA ELIMU YAKAGUA MIRADI YA MAENDELEO MANISPAA YA BUKOBA

    April 14, 2025
  • Angalia zote

Video

Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba akitoa maelezo juu ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Miradi ya Mbalimbali
  • Nyaraka mbalimbali
  • Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Tovuti kuu ya Takwimu Huria

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Bukoba Municipal Coucil

    Anwani ya Posta: P.O.BOX 284 Bukoba

    Telephone: +255 28 2220226

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: md@bukobamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki ©2017 Manispaa ya Bukoba .Haki zote Zimehifadhiwa